TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Monday, April 2, 2012

TANZANIA GOSPEL TEAM KUIBUA USHINDI BAADA YA KUITWANGA TIMU YA WAZO  4-3 

Mechi ilimechezwa leo katika uwanja wa Shule ya Kentoni Sinza Afrikasana. Timu zilionekana kuwa tishio uwanjani. Baada ya kipindi cah pili, fujo zikatokea uwanjani, mpira ulisimamihwa kwa kipindi kifupi na baadae mchezo ukaendelea. 

Mpiga picha, Rulea alichelewa kufika uwanjani mapema na hii imesababisha kutopata picha za pamoja za wachezaji....Tuanwaomba radhi wadau wetu wa Tanzania Gospel Team na wa Blogu yetu

Timu ya Tanzania Gospel ni hawa waliopiga uzi mweupe na timu ya Wazo ni wenye uzi wa kijani


Wachezaji wakilumbana
Kocha wa timu ya Gospel Team akiwaelekeza wachezaji 
 Mashabiki wa Tanzania Gospel Team wakichukua matukio
Kazi ikiendele


Mr. Kisaka akitoka uwanjani
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Emmanuel Mabisa (kulia) hakukosa uwanjani

Ukitaka video za mechi zinachochezwa na Gospel team unaweza kuwasiliana na bloggger, Rulea Sanga kwa simu +255 715 851523 au kwa email: rumatz2012@gmail.com