TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Wednesday, March 14, 2012

GOSPEL TEAM YAITWANGA VIBAYA TIMU YA PASI MIA BAO 4-2 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA KENTON SINZA AFRIKASANA-DAR LEO (Jumatano 14 Mach 2012)

Timu ya Gospel ilionekana kuchanganganyikiwa dakika za mwanzo katika kipindi cha kwanza ambapo walipigwa bao mbili kama wamesimama, na baada ya hapo mkono wa Mungu ukaingilia kati kwa watoto wake wa Gospel Team kwa kuwaliza mabao 4-2 . Mchezaji Ayubu wa Gospel Team alionekana kuwaburudisha sana wapenzi wa Gospel team baada ya kuingia kwa kumpokea Anani katika kipindi cha kwanza, alipopiga bao la kwanza, ambalo liliwapa nguvu wachezaji wa Gospel..

Tunaweza kusema Ayubu alifungua milango kwa Gospel Team. Wafungaji wengine ni Masele aliyefunga bao la pili, Mtangazaji wa Chanel Ten, Boniface Magupa alipiga bao la tatu na Francis kijana machachali sana alipiga bao la 4.

Mbali na uchezaji kulitokea vurugu kali kati ya wachezaji wa Pasi Mia na refarii, ambapo walimlalamikia kuwa anapendelea. Kutokana na vurugu hizo kuzidi Victor Aron alimuomba Anania kumsaidia Refarii huyo, lakini hakuwezekana kwa Anania kuwa refarii kwasababu alikuwa mchezaji na kubadilishana na Ayubu kipindi cha kwanza. Maoni yakapendekezwa kwa mfanyabiashara maarufu sana jiji Dar es Salaam, Zizzou kuwa refarii.

Mechi ikatulia na ikawa ya kufurahisha sana kutokana na refarii huyo kuwanyamazisha wachezaji na kuwaonya kuwa atayecheza fujo atatolewa nje ya uwanja.

Timu zikiwa fiti kuanza mpambano


Timu ya Tanzania Gospel Team ikiwa na kocha wao, Felix Msele (kulia)


Kazi imeanza


 Wachezaji walioko bench wakijiandaa kuingia, Geoge Mpella (kulia) akiwa ametulia

 Mchezaji wa Gospel Team na mtangzaji wa Praise Power Radio, Kisaka akiongea na blogger Rulea Sanga kuhusiana na ushindi 
 Blogger, Rulea Sanga aliyevalia Tshirt yenye msalaba akimsikiliza captain wa timu ya Gospel timu Yona Jakobo

 Kocha wa Gospel Team, Felix Masele (kulia) na kaptain wa timu hiyo, Yona Jakobo wakiteta jambo
 Mfungaji wa goli la kwanza wa Gospel Team, Ayubu akiwa ameshika kiuno akijiandaa kuingia uwanjani


No comments:

Post a Comment