TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Saturday, March 24, 2012



TANZANIA GOSPEL TEAM YATOKA UWANJANI VICHWA CHINI BAADA YA KUFUNGWA BAO 4-2 NA TIMU YA KOTA FC
Siku ya Jumamosi 25 Machi 2012 katika viwanja vya shule ya Kenton Sinza Mori, timu Kota FC waliwapiga bao 4-2 timu ya Tanzania Gospel bila ya huruma. 

Waliofungua milango ya mabo ni timu ya Kota FC ambayo ilitupia bao la kwanza katika kipindi cha kwanza dakika za mwanzo, na bao la pili lilipatikana katika kipindi hicho hicho. Tanzania Gospel waliamua kushambulia na kujipatia bao la kwanza katika kipindi cha kwanza na baadae kujipatia bao la pili kipindi cha pili. 

Mpaka mpira unaisha Kota FC walitoka na ushindi.....

Washindi KOTA FC 

Timu ya Tazania Gospel 
 Timu ya Kota FC iliyovali uzi wa njano
Mmmoja wa waratibu wa timu ya Tanzania Gospel Team kulia, George Mpela akionge na mchezaji wa TBC1 kuhusiana na mpambano wa leo
 Refalii akiwa na ma-captain wa timu
 Mwimbaji Datsun
 Tanzania Gospel Team wakifanya mazoezi kabla ya mechi
 Wachezaji na mashabiki wakiwa nje ya uwanja
 Goalkeeper  wa Tanzania Gospel
 Kota FC wakiwamsiliza mwalimu wao aliyevalia nyekundi kipindi cha kwanza
Mchezaji wa Kota FC akisaidiwa baada ya kuumizwa

Blogger  Papa Samsasal akiwacheki wachezaji
 Kazi inasonga
 Mabloga, kuanzia kulia Victor(www.hosannainc.blogspot.com), uncle Jimmy (www.unclejimmytemu.blogspot.com), Samsasali (www.samsasali.blogspot.com)



No comments:

Post a Comment