TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Saturday, March 17, 2012

GOSPEL TEAM YAITWANGA VIBAYA TIMU YA DAR CITY FC BAO 1-0 SIKU YA IJUMAA
Timu ya Tanzania Gospel iliondoka na ushindi wa bao moja ambalo lilipatika katika kipindi cha kwanza katika uwanja ya shule ya Kenton Sinza. Dar City hawakuamini kipigo walichokipokea kutoka kwa watumishi wa Mungu.
 
 Timu ya Tanzania Gospel

Timu ya Dar City FC 
 Goalkeeper wa Dar City FC haamini kilichopata baada ya mechi kuisha
 Kufungwa kunauma..angalia huyu mchezaji wa Dar City FC baada ya kipigo
 Goalkeeper wa Tanzania Gospel Team, Silas Mbise (wa pili kulia) akitafakari jinsi ya kuudaka mpira wa kona
Mambo yanasonga uwanjani 

Mratibu wa Gospel Tean, Erick Brighton (kulia) hakukosa

No comments:

Post a Comment