TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Friday, July 20, 2012

MECHI MBALIMBALI ZILIZOCHEZWA NA TANZANIA GOSPE TEAM

MECHI KALI KATI YA GOSPEL TEAM NA TUMAINI MEDIA TEAM ZIKIPAMBANA KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA KENTON SINZA MORI
7 March 2012
Mpigaji Picha: Rulea Sanga
Kikosi cha timu ya Gospel
 Kikosi cha timu ya Tumaini Media
 Refarii Hudson Kamoga akiongea na makepteni kabla ya mechi kuanza
 Timu ya Gospel na Tumaini zikiwasalimia kabla ya mechi kuanza
 Baadhi ya washabiki wakishuhudia mpambano
 Mtangazaji wa Praise Power, Deogras Pius (DP) kulia hakuwa mbali na mpambano.. na siku hii alikuwa daktari wa timu zote mbili
 Mfungaji wa goli la kwanza, Gerady (kulia)
 Mtangazaji wa Praise Power, Kisaka wa kwanza na anayefuatia ni mtumishi Stanle kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B
 Mwimbaji wa nyimbo za injili Jerry (kulia) na mtangazaji wa Praise Power Erick Brighton (katikati) na ndiye mratibu wa Gospel Team akiwacheki wana wakifanya mambo
Add caption
 Mzee wa Blogu na Creative Director wa kampuni yake inayoitwa Rumafrica and Africhina, akiwa amepigilia pamba zake za kumtukuza Mungu siku ya mechi. Na ndiye aliyezipiga hizi picha
Timu ya nje akisubiria kuingia ndani kupiga manyanga 
Goalkeeper wa Gospel Team akifanya mambo

---------------------------------------------------------
TIMU YA GOSPEL TEAM YATAMBA KATIKA UWANJA WA SHULE YA SKONDARI KENTON SINZA MORI BAADA YA KUITWANGA TIMU YA VANKHUVA MABAO 5-0
25 Feb 2012
Na mwandishi wenu, Rulea Sanga
Ni siku mbili zimepita, timu ya Gospel Team ilivyopiga bao timu ya Utumishi wa Umma kutoka ofisi ya Rais-Ikulu mabao 3-2, Jumamosi hii imegawa dozi tena kwa timu ya Vankhuva kwa kuwapiga mabao  5-0.  Wachezaji wa Gospel team walionekana kuwachanganya wapinzani wake kwa mbwembwe nyingi uwanjani  za kuwapiga chenga na washabiki kuzidi kuwazingua kwa mavuvuzela.
Baada ya mechi kuisha, makocha wa Gospel Team na Vankhuva Team  waliwasisitiza wachezaji wa pande mbili  kukaza buti kimazoezi na wasibweteke kwa haya mabao 5 na kujiona wamefika mwisho. Wachezaji waliyapokea hayo kwa mikono miwili na kuahidi kuwa watayatekeleza.
Gospel Team ni timu ambayo inajumuisha waimbaji wa nyimbo za injili, maproduza na watangazaji wa radio za Kikristo Tanzania. Lengo lao ni kumuinua Kristo kwa njia ya michezo na kuijenga na kuwaweka fit wachezaji kiafya. Mbali na hapo ni kujenga urafiki, kujuana na kuinua vipaji  kwa njia ya michezo. Mungu Ibariki Gospel Team
Wachezaji wa Gospel Team wakkimsikiliza mwalimu wao wa mazoezi.
Wachezaji wa Gospel Team wakipasha misuli kabla ya mechi
Timu ya Vankhuva wakiwa tayari kupambana na Gospel Team
 Gospel Team ikiwa na sura za mafanikio kabla ya mechi kuanza
Timu ya Vankhuva (jezi ya blue) wakisalimiana kabla ya mechi kuanza
Kazi imenza uwanjani...
 MC wa Glorious Celebration hakukosa kuliangalia pambano hili.
 Gospel Team wakiwa katika mapumziko kipindi cha kwanza
 Mzee wa Mablogu, Rulea sanga (wa pili kushoto) akiwa na goalkeeper wa Gospel Team, Silas Mbise.
Mbali na kuwa na uwezo wa kutengeneza blogu, pia ni mtalaamu wa shooting, movie editing, Graphic Design, Websites...huyu ni mzee anayejulika kwa mablogu, Rulea Sanga.
Mratibu wa Gospel Team, Erick (wa tatu kutoka kulia) akitafakari...
 Mtumishi kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, Stanley (kushoto), ambaye amekuwa msaada mkubwa katika timu ya Gospel kwa kuwatibu wachezaji wanaoumia uwanjani.
 Fulu kicheko, Mtangazjai na Meneja ya Praise Power Radio ( wa tatu kutoka kushoto) akifuatilia mpambano kipindi cha kwanza. 
 Mchezaji wa Vankhuva aliyeumiza baada ya mchezaji wa Gospel team, George Mpela kuvaa kwa bahati mbaya sehemu ya ugoko.
 Hiki ni kidonda...Tunaomba maombezi yako kwa huyu mchezaji, kwani ilikuwa bahati mbaya uwanjani
 Wachezaji wa pande mbili wakipigwa picha ya pamoja baada ya mechi kuisha
MUNGU IBARIKI GOSPEL TEAM NA VANKHUVA TEAM..AMEN
------------------------------------------------------------------------
BREAKING NEWS
GOSPEL TEAM YA FOOTBALL YAWAPA KIPIGO KILICHOENDA SHULE TIMU YA UTUMISHI WA UMMA KUTOKA OFISI YA RAISI MABO 3-2

WAKATI HUO HUO TIMU YA NETBALL YA GOSPEL TEAM YAPEWA KIPIGO KITAKATIFU NA TIMU YA UTUMISHI WA UMMA KUTOKA OFISI YA RAISI MABAO 23-16

MECHI ZILICHEZWA KATIKA UWANJA WA SHULE YA KENTON SINZA MORI TAREHE 23 FEB 2012
Timu ya Utumishi ofisi ya raisi yatoka uwanja huku ikiinamisha vichwa chini baada ya kupata kipigo kikali kwa kupigwa mabao 3-2 na Gospel Team.  Timu ya Gospel Team ilianza kutikisa nyavu kipindi cha kwanza. Wachezaji wa pande mbili walionekana machachari sana vipindi vyote viwili, kwani kila mmoja alitaka kutoka na ushindi. Mungu alionekana kuwatetea watoto wake wa Gospel Team kwa kuwapa ushindi.
Mchezaji wa Gospel Team, Elisha alionekana nyota inayong'aa katika uwanja kwa uchezaji wake mzuri.
Wakati huohuo dada zetu wa Gospel team waliabishwa na timu ya Utumishi wa Umma kutoka ofisi ya Rais baada ya kupata kichapo kitakatifu cha mabao 23-16. Lakini jina la BWANA linazidi kutukuzwa. 
Baada ya Mechi kuisha Gospel Team ilifunga ukurasa kwa nyimbo na maombi makali ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi hilo. 
 Timu ya Netball kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma  kabla  ya mech kuanza
 Timu ya Netball ya Gospel Team ikiwa katika pozi kabla ya mechi kuanza
Refarii wa katikati akiwapa maelekezo kabla ya mechi kuanza
Kazi imeanza
 
 Timu ya  Football ya Gospel Team kabla ya mechi kuanza..Bado wamepiga pamba za mazoezi
Timu kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma akiwa katika pozi kali kabla ya timu kuanza
 Watangazaji wa Praise Power Radio, Erick Brighton (kulia), George Mpella (katikati) na Victor Aron na pembeni yake ni mwanae..wakipasha kabla ya kuanza mechi
 Watangazaji wa Praise Power wakiuangalia mpira waliozawadiwa na mtangazaji wa Clouds FM, George Njogopa
 Kazi imenza...maji yametimuliwa
 Refarii wetu alikuwa Hudson Kamoga, Mtangazaji wa Praise Power
 Goalkeeper wa Gospel Team, Silase Mbise akiwapanga mabeki wake
Baadhi ya wachezaji waliokuwa bench wakiwa na kocha wao (aliyevalia shart la kijani)
Hata mzee wa mablogu, Rulea Sanga (kushoto) alikuwepo uwanjani baada ya kutoka kijijini kwake Mtili A, Mufindi..angalia akishangaa timu za mjini...mshamba huyooooooo.....
------------------------------------------------------
TIMU YA WAIMBAJI, MAPROMOTA NA WATANGAZAJI WA RADIO ZA KIKRISTO WAKIWA KATIKA MAZOEZI-SHULE YA KENTON SINZA 
Timu hii inafanya mazoezi tayari kupambana na timu mbalimbali ndani ya jiji la Dar es Salaam na mikoani ndani ya mwezi Februari. Mtapewa taarifa kwa kupitia blog hiin na kwa kusikiliza Praise Power Radio 99.2FM
 Wadada wa Yesu wakifanya mazoezi
 Timu imekamilika. hakuna cha wadada wa nani...mambo yanasonga
 Dada yetu ambaye jina lake mhalikupatikana akitokea Uganda akifanya mahojiano na meneja wa radio ya Praise Power
 Mwimbaji wa nyimbo za injili, Makondeko akipiga ung'eng'e (kiingereza) na dada kutokea Uganda aliyefika uwanjani hapo kushuhudia mazoezi
 Makondeko mwenye kikaushi cheupe akiutafuta mpiran kwa hamu
 Meneja wa Radio ya Praise Power na Mtangazaji, George Mpera akipata matibabu baada ya kuumia mguu
 Makondeko akiukimbiza mpira
 Kiongozi wa nidhamu wa timu, Noel Tenga akifanya mambo yake katika mtandao wakati wa mazoezi
 Mzee wa mablogu na meneja wa kampuni ya RUMAAFRICA & AFRICHINA, Rulea Sanga, kulia akiwa na marafiki zake (kutoka kushoto ni George Mpella, rafiki, Erck Brighton)
 Wachezaji wakikosoana baad ya mazoezi kuisha
Kiongozi wa timu iliyoko Kinondoni (aliyevaa kofia) akiwaomba wachezaji kufanya mechi na timu yake
--------------------------------------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------
WATANGAZAJI, WAIMBAJI NA MAPROMOTERS WA INJILI TANZANIA WAKIJIFUA TAYARI KUPAMBANA NA TIMU YA BONGO MOVIE ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI, 28 JANUARY 2012
Mechi hii itachezwa katika viwanja vya TTCL/POSTA Kijitonyama (Science) ambapo kutakuwa natamasha la uimbaji baada ya mechi kuisha. Waimbaji kama Bony Mwaitege, Flora Mbasha, Bahati Bukuku, Mzee wa nyimbo ya zungukazunguka atakuwa ndani ya uwanja, na waimbaji kibao. Kutakuwa na kiingilio cha buku tano (5000/=) mlangoni, kama utataka tiketi, jisogeze maeneo ya Efatha Mwenge, Ubungo Oil Com. Mechi itaanza saa 6:00 mchna. Utakutana na waigizaji wa filamu za Kibongo kama JB, Ray, Kanuba, Irene Uwoya, Wema Sepetu, na wengine wengi.
Angalia maandalizi  haya:
Wtangazaji wa Praise Power Radio, BP (aliyekaa) na Uncle Jimmy wakijadili jambo kabla ya mazoezo kuanza
BIG..George Mpela akipiga kipenga kuwaita wachezaji uwanjani
Fuuuuuuuuulu shangwe na Bony Magupa wa macheliiiiiii...mtangazaji wa Channel Ten
Kiuno kaka..haya yalisemwa na BIG George Mpela (aliyevalia jezi ya yelow...akiwa na mzee wa mablogi Rulea Sanga (RUMA)
"Watumishi hilo zoezi ni noma..sifanyi hata kwa dawa..." Big George Mpella
Majambozi yanendelea
Mtangazaji wa Channel Ten Bony Magupa (kulia) akiwa na Mzee mzima Big-Mtangazaji wa Praise Power, George Mpella..wakitroti....
Kazi inasonga
------------------------------------------------------


MAZOEZI YAMEPAMBA MOTO KWA MAPROMOTA, WATANGAZAJI NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TAYARI KUKABILIA NA TIMU YA BONGO MOVIE SIKU YA KESHO JUMA JUMAMOSI...
Watangazaji wa Praise Power wakiwa tayari kulianzisha boli 
 Mwimbaji Bony Mwaitege aliyevalia tarck na yuko kifua wazi akitafuta position
 Mchekeshaji Chavala (kulia) akiongea na baadhi ya wachezaji
 Wachezaji wakimsiliza kocha wao
Mwimbaji wa nyimbo za injili Bony Mwaitege akiwaweka sawa wachezaji wenzake kwa kuelezea baadhi ya madhaifu aliyoyaona.
 Wachezaji wakipata mawaidha kutoka kwa viongozi wao
 Blogger Rulea Sanga (alishika mpira) na yeye alikuwapo
Msikilizaji mkubwa wa Praise Power, Mama Abuu akiongea na wachezaji akiwemo Mtangazaji wa Praise Power Victor Haron (anayevaa soksi)
Kazi inasonga
Mzee wa Mablogi na website na grfix, Rulea Sanga akitoa huduma ya kwanza kwa mtangazaji wa Praise Power, Kisaka.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Musa Shabani akiwa na furaha ya kufa mtuac
Graphic Designer Rulea Sanga akimchua mchekeshaji wa Gospel, Chavala..baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi

-------------------------------------------------------------


MECHI KATI YA WATANGAZAJI WA RADIO NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LAFANA KATIKA VIWANJA VYA TTCL- KIJITONYAMA.
Siku iliyokuwa inasubiriwa na Watanzania kuhusiana na mechi kali kati ya Watangazaji, mapromota na waimbaji wa nyimbo za injili waliotegemea kupambana na wacheza filamu (Bongo Movie). Zoezi hili  halikuweza kufanikiwa kutokana timu ya Bongo Movie kuwa na mualiko Zanzibar katika tamasha lao la ZIFF. Badala yake kamati iliamua kupambanisha kati ya Waimbaji wa nyimbo za injili na Watangazaji wa radio za kikriso Tanzania. 
Tamasha lilionekana kuvutiwa na Watanzania wengi. Timu ya Watangazaji ilipigwa bao 2 na Waimbaji kuibuka washindi kwa mabao 5. Mfungaji bora wa watangazaji alikuwa Mtangazaji wa Channel Ten ambaye alikuwa mtangazaji wa radio ya  Praise Power, Boniface Magupa aliyefunga mabao mawili na kujipatia Tsh. 5000 kama mfungaji bora.
Mbali na mashindano ya mpira ya miguu kulikuwa na mchezo wa kufukuza kuku ambapo Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore alijishindia kuku na upande wa watangazaji wa radio, Yusuf Magupa wa Praise Power alishinda na kujipatia kitoeo cha kuku.
Waimbaji kama Martha Mwaipaja, Martha Ramadhan, Glorious Celebration na wengine wengi walionekana kugusa mioyo ya watu kwa  nyimbo zao zenye kumwinua Mungu wetu.
 Baadhi wa wachezaji wakiwa katika kiwanja cha shule ya Kenton Sinza wakijiandaa kuelekea katika uwanja wa Posta-Kijitonyama.
Stori zikiendelea.....
 Timu ya waimbaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Kenton Sinza
 Timu ya Watangazaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Shule ya Kenton, Sinza
WACHEZAJI WAKIWA KATIKA UWANJA WA POSTA KIJITONYAMA
Bony Mwaitege (aliyevalia jessy nyeupe) akiufuatilia mpira
Goolkeeper wa watangazaji kutoka radio ya Praise Power, DP akiwa ameshikilia bori baad ya kufungwa.
MC  Uncle Jimmy
 Kipindi cha kujitambulisha
 Mashabiki
 Mtangazaji Kisaka
 Kipindi cha mapumziko
 Timu ya Waimbaji katika kipindi cha mapumziko
 Msikilizaji maarufu wa Praise Power a.k.a Mzee wa Kubonya
 Mtangazaji wa Praise Power (kulia), Uncle Jimmy na Mchekeshaji Chavala (kushoto)
 Mzee wa mblogu na mawebsite pamoja na mgarphics, Rulea Sanga (katikati akiwa amezungukwa na waimbaji wa Glorious Celebration
Mtangazaji wa Wapo Radio, Silas Mbise (kulia) akiwa na rafiki zake. Kutoka kushoto ni Jessica na lilian
Watangazaji wa mpira wakiwa katika corner yao
 Waimbakji wa Glorious Celebration wakitoa huduma yao ya juimbaji katika pambalo la mpira
Glorious Celebration Live Band
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore (anayepunga mkono), akiwaongoza waimbaji wenzake baada ya kushuka jukwani
Martha Mwaipaja

No comments:

Post a Comment