TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Monday, May 7, 2012


"GET TOGETHER PARTY" KUFANA LEO KATIKA  HOTELI YA ERICK SHIGONGO -"THE ATRIUMS"- SINZA AFRIKASANA-DAR

KIKAO CHA MALIZIKA JANA KUHUSU "PARTY YA GET TOGETHER"
Kutakuwa hakuna kiingilio kwa kila mtu atayefika mahali pale. Hii ni party inayowashirikisha watu wote wanaompenda Mungu na kutakuwa na uimbaji kutoka kwa waimbaji wa injili mbalimbali. 

Utapata muda wa kuonana na waimbaji wa nyimbo za injili, maproducer, mabloggers, watangazaji wa radio za injili, wachekeshaji, wajasiliamali, baadhi ya wachungaji. Mbali na kuona utwasikia nini wanakifanya katika sekta zao.

Pia kutakuwa na "SURPICE" ambayo itakufanya ubaki mdomo wazi na kutosahau hicho kitu kitakachotokea mahali hapo siku ya leo.

Party itaanza saa 12:00 jioni na hakuna kiingilio. Utapata chakula cha kutosha kutoka kwa wahudumu wa "The Atriums Hotel" kwa bei nafuu sana.

Party itakuwezesha wewe kufahamiana na watu na kuwezesha wewe kupata "Connection" na watu ambao ulikuwa huwajui. Kumbuka kuja na business card yako kwaajili ya kugawa mawasiliano kwa yule utayekutana naye.

Mimi nikutakie siku njema na usikose kuja na ngugu na jamaa zako !!!!!!!!

 Kamati ya maandalizi: Erick Brighton, Rulea Sanga, Lister, Kisaka, Noel Tenga, Boniface Magupa, Makondeko




Blogger, Rulea Sanga akitokelezea katika kikao

No comments:

Post a Comment