TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Saturday, May 5, 2012

"GETHER TOGETHER PARTY"  KWA WAPENDWA WA MUNGU


 ----Party ambayo haijawahi kutokea Tanzania kwa wapendwa na watu wote wanaolichini ya angaa hii wenye mapenzi mema na Mungu na wenye hofu ya Mungu----

Watu watapata kubadilishana mawazo, kujuana na kujua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Kutakuwa na nyimbo za injili na band zitapiga muziki "Live" na kutakuwa na "surprise" ambayo utakumbana nayo siku hiyo. Siku hiyo itakuwa ni siku ya kusifu na kumchezea Mungu.

Utapata muda wa kuonana na ma-producer wa nyimbo za injili, waimbaji, timu ya Gospel Team, Mabloggers wa blogu zinazomtangaza Yesu Kristo, Watangazaji wa nyimbo za injili, wapigaji maarufu wa simu katika vituo vya radio za injili Tanzania, Salamu kutoka kwa bloggers waliopata bahati ya kualikwa Nigeria kwa Nabii TB Joshua, Wachekeshaji, na mengine mengi.

Party itafanyika: siku ya Jumanne 8 Mei 2012
Muda:                 1:00 jioni
Eneo:                  The Atriums Hotel, Sinza Afrikasana, Dar es Salaam- Tanzania

No comments:

Post a Comment