TANZANIA GOSPEL TEAM

Tanzania Gospel Team ni timu ya mpira wa miguu (football) na mpira wa mikono (netball). Timu hii iko nchini Tanzania mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kinondoni, Sinza Afrikasana.

Timu imejumuhisha wachezaji kutoka makanisa mbalimbali ya Kikristo na hasa waimbaji, maproduza na watangazji wa radio za kikristo.

Lengo la kuanzisha timu hizi ni kumtangaza Kristo kwa njia ya michezo, kuwaunganisha wapendwa wa Bwana kutoka makanisa mbalimbali, kuweka urafiki na undugu, kuijenga miili ya wachezaji kiafya, kuburudisha, kuonyesha mshikamano na ushirikiano kati yetu, kujuana na kufahamiana.

Tangia timu ianze januari 2012 kumekuwa na maendeleo mazuri na watu wengi wamekuwa wakifika katika viwanja vyetu vya mazoezi vilivyooko Sinza Afrikasana katika shule ya Kentoni.  Mungu ametuwezesha kucheza na timu mbalimbali kama vile Dar City FC, Walabata, Pasi Mia, na zingine nyingi.

Tunaomba sana maombi yako ili tuweze kuwa na mafanikio kwa kucheza na timu kubwa kama Manchester, Arsenal, Liverpool, Yanga, Simba n.k

Tunaamini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.  

Sunday, May 20, 2012



TANZANIA WORSHIP EXPERINCE WAKIWA WAPO RADIO KUHAMASISHA WATU KUJIANDIKISHA KATIKA SAKATA LA KUWATAFUTA WATU WENYE UWEZO WA KUIMBA NYIMBO ZA KUABUDU
Wakihojiwa na mtangazaji wa Wapo Radio Joyce, wamesema kwa neema ya Mungu wamejipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa haki. Mchungaji Charles Mbogoma amehimiza watu kufika kwa wingi siku ya jumamosi tarehe 26 Mei 2012 katika hoteli ya The Atriums iliyoko Sinza Afrikasana Dar es Salaam.

Naye Blooger Rulea Sanga amesema anahakikisha matukio yote yatakayokuwa yanatokea yatarushwa katika mitandao mbalimbali na katika radios na TV. Amesema kwa sasa unaweza kutembelea katika blogu hizi www.rumaafrica.blogspot.com au www.tanzaniaworshipexperience.blogspot.com

Makalanga alisema unaweza kujaza form ambazo zipo katika ofisi ya Unversal Inc maeneo ya Posta au ingia katika blogu ya www.tanzaniaworshipexperience.blogspot.com

MNAKARIBISHWA WOTE HAKUNA KIINGILIO CHOCHOTE. HATA KAMA HUJUIKUIMBA UNAKARIBISHWA
 Mmoja wa judges, Emmanuel Mabisa
 Logistic na Katibu, Nasobile (kulia), akifuatia Mch. Mbogoma
 Mtangazaji wa Wapo Radio, Joyce
IT na blogger Rulea Sanga wa pili kutoka kushoto 
 Mchungaji Charles Mbogoma
 Mwenyekiti, Mkalanga

 Blogger na IT, Rulea Sanga
JAZA FOMU HII KUJIUNGA

TAFADHALI TUMA BARUA PEPE KWETU YENYE MAJIBU YA MASWALI YALIYOULIZWA HAPO CHINI:

NB: Soma kwa makini na ukishasoma nakili mahali fulani majibu yako na utume kwetu kwa kutumia barua pepe hizi hapa chini: Tafadhali tuma majibu yako kwa barua pepe (email) zote hapo chini. Unaweza kubofya katika email mmojawapo na ukaanza kujaza fomu yako. Angali mfano hapo chini ya maswali.

1. JINA LA KWANZA----------------------
2. JINALA LA UKOO---------------------
3. ANUANI YAKO------------------------
4. NAMBA YA SIMU--------------------
5. UMRI--------------------------------------
6. JINSIA YAKO-------------------------
7. TAREHE YA KUZALIWA: TAREHE-----MWEZI---MWAKA
8. KANISA LAKO-----------------------
9. JINA LA MCHUNGAJI WAKO-----------------------
10. ANUANI ZA MCHUNGAJI WAKO: 
      SIMU-----------BARUA PEPE--------------------
11. UMEOKOKA?: NDIYO:--------HAPANA:----------
12. LINI UMEBATIZWA?: 
      TAREHE-------MWEZI------MWAKA
13. LINI UMEJAZA ROHO MTAKATIFU?:
      TAREHE------------MWEZI----------MWAKA
14. UNAJUA MAANA YA KUABUDU: 
      NDIYO----------------HAPANA----------
15. MKOA UNAOTOKA-------WILAYA-----

Sasa tuma majibu yako kwa tumia barua pepe hizi:
MFANO WA KUJIBU:
Jina la kwanza: Rulea
Jina la ukoo: Sanga
Anwanuani: Box 120 Dar
Namba ya simu: 0715851523
Umri: 12
Jinsia: mwanaume
Tarehe ya kuzaliwa: 30 Juni 1990
Kanisa langu: Mlima wa Moto Mikocheni B
Mchungaji wangu: Dr Getrude Rwakatare
Anwani ya mchungaji wangu: Box 234 Dar, 
          Simu: 0715851523 Barua pepe: info@rwakatare.com
Ndiyo nimeokoka
Tarehe ya kubatizwa: 20 Juni 2011
Ndiyo nimejazwa : Tarehe 30 Septemba 2011
Tarehe ya kupokea: Roho Mtakatifu: Tarehe 30 Septemba 2011
Sijui maana ya Kuabudu lakini naweza kuimba kutokana na kuwa nina sauti nzuri na hisia kali

AHSANTENI

KIINGEREZA
First name...................................Second name................

Address........................cell number..........
Age......................
Sex.....................
Bon again..............yes........no........
Your church................
Your pastors contact................
When were you buptized................
When were you filled with the holly spirit.............
do you know the meaning of worship...............

John 4:24

No comments:

Post a Comment